Okoa Maziwa Ongeza Mapato
Loading...
Date
2017
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Kenya Agricultural and Livestock Research Organization
Abstract
Ndama hukua pole pole (chini ya gram 300 kwa siku) na hufa kwa wingi (asilimia15-20) kwa sababu ya ukosefu wa lishe bora. Wafugaji hukosa kuwapa ndama maziwa ya kutosha ili kujiongezea faida kutokana na maziwa. Ndama huhitaji lita (L) 400 za maziwa toka kuzaliwa hadi kuachishwa maziwa. Gharama yake ni Ksh 16,000 kwa bei ya Ksh 40 kwa lita. Nusu ya kiasi hiki cha maziwa chaweza kusalia na kuuzwa ikiwa kitabadilishwa na uji wa mahindi kunde na maziwa. Uji huu waweza kutumika palipo na kunde. Maharagwe yaweza kutumika badala ya kunde katika sehemu za miinuko.
Description
Keywords
ndama, maziwa, uji wa mahindi
Citation
Mwanachi, D.M. & Bimbuzi, S. (2017). Okoa Maziwa Ongeza Mapato [Brochure]. Kenya Agricultural and Livestock Research Organization